PSG YAWAFUKUZIA YAYA TOURE, BASTIAN SCHWENSTEIGER

 MIAMBA ya soka ya Ufaransa klabu ya PSG ipo kwenye mipango ya kuhakikisha inazinasa saini za viungo wakongwe Yaya Toure na Bastian Schwensteiger ifikapo Januari mwakani kwenye dirisha dogo la usajili.

Nafasi za viungo hao kwenye klabu zao za Manchester City na Manchester United ni finyu kwa sasa na wapo huru kuzihama timu zao hizo wakati wowote.


PSG ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa “Ligue 1”, wamedhamiria kutoa ofa ya pauni mil 1.5 kwa kila mmoja ili kujiongezea nguvu ya kutetea ubingwa msimu huu.

No comments