Habari

RANIERI AWASIHI MASHABIKI WA “THE FOX” KUMPOKEA KANTE KWA MIKONO MIWILI

on

KABLA ya Leicester City kucheza
na Chelsea, meneja wa klabu hiyo, Claudio Ranieri aliwasihi mashabiki wa The
Fox kumpokea kwa mikono miwili kiungo kutoka nchini Ufaransa, N’Golo Kante
ambaye alirejea klabuni hapo akiwa na kikosi cha Chelsea.
Ranieri aliwasilisha ombi hilo
kwa mashabiki kufuatia kikosi cha Chelsea kutarajia kucheza mchezo wa Kombe la
Ligi (EFL) dhidi ya Leicester katika uwanja wa King Power.
Kante aliondoka klabuni hapo
wakati wa usajili wa majira ya kiangazi na kujiunga na klabu ya Chelsea, jambo
ambalo linachukuliwa na mashabiki kama aliisaliti Leicester ambapo bado ilikuwa
inamwitaji katika kipindi hiki cha kutetea taji lao hilo.
“Ninafarijika kuona Kante
anarejea tena hapa na nitampokea kwa furaha na bashasha kutokana na mahusiano
yetu kuwa mazuri tangu nilipomsajili mwaka 2015 akitokea Caen.”
“Ninataka kuona hata kwa mashabiki
inakuwa hivyo kwa sababu Kante bado ni sehemu ya familia yetu, ambaye
alionyesha kujituma na kupata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Ligi msimu
uliopita.”
“Mashabiki wanapaswa kufahamu
kwamba soka ni mchezo ambao una changamoto zake na wakati mwingine inakuwa
ngumu kuamini kwamba mtu anaweza kukuacha katika kipindi unachomwitaji, lakini
bado ninasisitiza Kante ni mwenzetu na tunapaswa kumuheshimu kwa kiasi kikubwa,”
alisema Ranieri.
Kante alikuwa mchezaji pekee
aliyeamua kuondoka wakati wa majira ya kiangazi, huku wachezaji wenzake
waliochangia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa England msimu wa 2015/16, Jamie Vardy
na Riyad Mahrez, wakikubali kusaini mikataba mipya.

Klabu ya Arsenal ilionyesha nia
ya kutaka kuwasajili Jamie Vardy na Riyad Mahrez lakini bado msimamo wao
ulidhihirisha mapenzi na Leicester City.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *