RAY KIGOSI AJITETEA KUHUSU LAWAMA ZA KUWA NA "MAPOZI" KWA WASANII CHIPUKIZI

MWIGIZAJI Vincent Kigosi "Ray" amefunguka na kusema kuwa yeye hana maringo kama ambavyo amekuwa akituhumiwa na baadhi ya watu kutokana na msimamo wake wa kutoshiriki katika filamu za wenzake.

Alisema kuwa amekuwa anaonewa bure na kwamba yeye siyo mtu wa aina hiyo bali kinachomfanya wakati mwingine ashindwe kushiriki filamu za wenzake ni majukumu yake muhimu.


“Mimi siko hivyo, sina pozi lakini nina majukumu mengi si kama inavyodaiwa kuwa mimi nina pozi ila huwa ninashindwa kushiriki kwenye filamu za wasanii wanaochipukia kwa sababu ya majukumu yangu mengine,” alisema Ray.

No comments