RAYMOND WA "WASAFI" ASEMA HANA UGOMVI NA WEMA NA ALIMTAKA KWENYE VIDEO YA "NATAFUTA KIKI"

MSANII wa Bongofleva kutokas WCB Raymond ambaye anatamba na video yake ya "Natafuta Kiki" ambayo ndani yake mastaa kibao wametokelezea, amesema kuwa hakutaka video hiyo itoke bila ya Sura ya Wema Sepetu.

Raimond anasema wakati anashooti video hiyo Wema alikuwa busy kwa hiyo ikabidi achukue moja ya clip walizowahi kushoot wakiwa pamoja kwenye barthday ya Romy Jons.

“Mimi sima ugomvi na Wema ndio maana hata nilipomuona kwenye party ya Romy nikaenda kumsalimia na Camera Man wakachukua Video," alisema Raymond.

"Mwanzoni nilishaongea naye kuhusu yeye kutokea kwenye video ya Natafuta Kiki lakini ratiba zake zikambana mimi nilishasema moyoni mwangu natanani nione sura ya Wema kwenye Natafuta Kiki, kwahiyo nikawa sina jinsi,” alifunguka. Ray.

No comments