REAL MADRID YAKATAA OFA ZOTE KUMUHUSU JAMES RODRIGUEZ

WAKATI ambapo James Rodriguez anahusishwa na tetesi za kutaka kutua kwa Mashetani wekundu wa jiji la Manchester, klabu yake ya Real Madrid imekataa ofa yoyote.  

Rodriguez mwenye umri wa miaka 25, amekuwa na mafanikio ya wastani tangu atue mwaka 2014 katika kikosi cha Los Blancos.

Ameifungia Real Madrid jumla ya mabao 21 katika michezo 58 ambayo alipangwa ikiwa ni pamoja na ile mara 32 ya michuano ya ndani La Liga.

Akinukuliwa juu ya kumkatalia kuondoka, kocha Zinedine Zidane alisema: “Rodriguez ni mchezaji muhimu ndani ya Real Madrid.”

“Tetesi za sasa ni kupuuzwa kwani Real Madrid haina mpango wa kuachana na straika huyu.”

“Tunatambua kuwa Manchester United na Chelsea wamo mbioni kutaka saini yake, lakini nimekaa na Rodriguez na kukubaliana baadhi ya mambo.”


“Nimemwakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza, nimemwambia bado ninaendelea kumwamini.”

No comments