Habari

RIHANNA SASA KUSAIDIA WATOTO KATIKA SUALA LA ELIMU DUNIANI

on

MWANAMUZIKI wa R&B duniani,
Rihanna anapenda watoto waende shule. Taasisi yake ya “Clara Lionel Foundation”
imeungana na Global Partnership For Education And Global Citizen katika mradi
wa miaka mingi wa kusaidia elimu duniani.
Kupitia mradi huu, Rihanna ana
matumaini ya kuwatetea watoto zaidi ya robo bilioni ambao hawako shuleni pamoja
na wanafunzi mil 330 ambao hawajifunzi kitu katika shule walizopo.
Akiwa kama balozi mpya wa dunia
wa GPE, Rihanna anatarajiwa kufika katika nchi zinazoendelea zaidi ya 60, akizipa
kipaumbele zile zenye uhitaji zaidi zikiwemo zenye migogoro. Tanzania ni moja
kati ya nchi zenye changamoto kubwa za elimu.  
   
Mwenyekiti wa GPE, waziri mkuu
wa zamani wa Australia, Julia Gilard amesema anayo furaha kubwa kuingia
ushirikiano na Rihanna ambaye jina lake halisi ni Robyn Fenty.

Rihanna alianzisha Clara Lionel
Foundation mwaka 2012 kwa kumbukumbu ya bibi na babu yake Clara na Lionel
Braithwaite.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *