ROBERTO MARTINEZ ACHEKELEA UBERGIJI KUUA CYPRUS 3-0

KOCHA Roberto Martinez licha kuwa anafahamu bado ana kazi kubwa ya kufanya katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ubergji, amesema kuwa amefurahi kuanza kuona mabadiliko baada ya timu yake kuondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Cyprus hivi karibuni.

Ubelji imeanza vizuri michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia baada ya staa wao Romelu Lukaku kupachika mabao kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliopigwa mjini Nicosia na Yannick Carrasco akiongeza la tatu dakika za mwisho.

Kabla ya kupata ushindi huo kulikuwepo na vilio na kuzomewa baada ya kufungwa katika mechi yake ya kwanza Maretnez katika mchezo wa kirafiki ilipolala kwa mabao 2-0 dhidi ya Hispania, lakina kwa sasa kocha huyo wa zamani wa Everton anaonekana kuanza kufurahi.

“Hatukutarajia mechi kuwa rahisi katika hali ngumu kama hii, lakini tumeweza kupata mabao matatu, tukakosa penati na nafasi chache,” kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari.

Aliusifu ukuta wake kwa kutoruhusu bao na akasema kwamba atauimarisha zaidi. 

No comments