CRISTIANO RONALDO ameonyesha kuchukizwa baada ya kocha Zinedine Zidane  kumpiga benchi katika mchezo wa La Liga wa sare ya 2-2 dhidi ya Las Palmas.
Mchezaji huyo wa mwaka wa FIFA alishangaa pale alipotakiwa kwenda benchi dakika ya 72 hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kumtokea ndani ya miaka saba iliyopita.

Zidane alimpumzisha Ronaldo kwa sababu za kiufundi lakini badala ya kusaidia, hatua hiyo ikamwadhibu kwa kuruhusu La Palmas kufunga bao la kuzawazisha ukingoni mwa mchezo.

Sergio Araujo nyota wa zamani wa Barcelona B ndiye aliyefunga bao hilo la kusawazisha dakika ya 85.

Real Madrid ilifunga bao la kwanza dakika ya 33 kupitia kwa 
Marco Asensio lakini La Palmas wakasawazisha dakika mbili baadae mfungaji akiwa ni Tana.

Karim Benzema akaipa Real Madrid bao la pili kunako dakika ya 67 ambalo lilidumu hadi dakika ya 85.

NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac