ROONEY ALIJIANDAA KUTOSWA NA MOURINHO KIKOSI CHA KWANZA MAN UNITED

WAYNE Rooney alijiandaa kutoswa na kocha Jose Mourinho katika kikosi cha kwanza cha Manchester United kutokana na kucheza chini ya kiwango mfululizo.

Hata hivyo nahodha huyo wa United na England alicheza dakika zote tisini za mchezo wa EFL Cup dhidi ya Northampton Town uliochezwa Jumatano usiku.

Katika mchezo huo ambao United ilishinda 3-1, Rooney hakuonyesha soka la kuvutia hali inayozidi kumweka mashakani kwenye michezo ijayo.

Duru za michezo nchini England zinaamini kuwa Rooney ameanza kuhofia kusugua benchi chini ya Mourinho.

No comments