ROSE NDAUKA AKIRI KUWEPO NA MAKAHABA BONGOMUVI

MSANII wa filamu Rose Ndauka amefunguka na kuweka wazi kuwa kuna wasanii wachache wa kike kwenye tasnia hiyo ambao wanaichafua kwa vitendo vyao vya kujiuza.

“Sio kila msanii anayeingia kwenye filamu anataka kupata wanaume lakini wapo baadhi wasanii hukumwa na hivyo kusababisha Bongomovies kuonekana ya wahuni,” alisema.

Alifafanua kitendo cha wanawake kujiuza sio kwenye tasnia ya filamu tu bali hata katika maisha ya kawaida wapo watu wa aina hiyo na kwamba sababu kubwa ni hulka ya mtu. 


“Tabia hii haitokani na kuwa kwenye filamu bali ni hulka tu ya mtu ambayo inasababisha jamii iamini kwamba watu wote ni wahuni na kumbe hakuna ukweli wowote.

No comments