ROY KEANE AMPONDA JOSE MOURINHO NA KUMFAGILIA PEP GUARDIOLA

NYOTA wa zamani Roy Keane amemmwagia sifa kocha wa Manchester City, Pep Guardiola akisema kuwa yeye ndiye Special One wa ukweli na wala si wa Manchester United, Jose Mourinho.

Usiku wa kuamkia juzi Guardiola alifikisha mechi yake ya saba akishanda tangu alipotua kwenye klabu hiyo ya Etihad wakati ilipoinyuka Borussia Monchengladbach kwa mabao 4-0 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Akiwa Chelsea mwaka 2004, Mourinho alikuwa akijitangaza kuwa anavyodhani yeye ndiye Special one mwishoni, mwa wiki akaambilia kipigo chake cha kwanza wakati waliponyukwa na Man City kwa mabao 2-1 katika michuano ya Ligi Kuuu England.

Kutokana na matokeo hayo Keane ambaye anatarajia Man City kuendelea kung’ara msimu huu anasema kiuwa Guardiola ni mkali kuliko mwenzake huyo wa Old Trafford.

“Kwa makocha hao wawili wa jiji la Manchester, Mourinho amekuwa akijiiita Special One lakini kwangu mimi anayestahili ni Guardiola,” alisema mkongwe huyo.

No comments