Habari

SAM ALLARDYCE ABWAGA MANYANGA TIMU YA TAIFA ENGLAND … Gareth Southgate akabidhiwa mikoba

on

Allardyce's sacking means he is the shortest-serving permanent England manager in history
KOCHA wa England Sam Allardyce amejiuzulu nafasi hiyo kufutia tuhuma zilizoibuliwa na gazeti la Daily Telegraph la nchini humo, chama cha soka cha Engalnd FA kimethibisha.
Sam Allardyce ambaye ni kocha wa zamani wa Sunderland  ameachia nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa siku 67 tu.

Uchunguzi wa gazeti la Daily Telegraph unasema kuwa Allardyce mwenye umri wa miaka 61,alitumia cheo chake kushauriana mpango wa pauni 400,000 na kutoa ushauri kuhusu vile anaweza ”kuzunguka” sheria za uhamiaji wa wachezaji.

Kwa mujibu wa Daily Telegraph, Allardyce maarufu kama Big Sam pia amelikosoa shirikisho la soka nchini Uingereza FA, kocha aliyemrithi Roy Hodgson, na msaidizi wake Gary Neville.

Kama ilivyobashiriwa, Gareth Southgate amerithi  nafasi hiyo kwa muda katika mechi zijazo dhidi ya Malta na Slovenia.

Taarifa kamili ya FA ni hii hapa:

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *