SCHOLES AZIDI KUSISITIZA UJIO WA IBRAHIMOVIC MAN UNITED UNA FAIDA KUBWA

PAUL Scholes amesisitiza kuwa ujio wa Zlatan Ibrahimvic Man United utakuwa na faida kubwa kwa mustakabali wa Marcus Rashford.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden aliwasili Old Trafford majira ya joto na ameanza vyema kibarua chake Man United kwa mabao manne kwa mechi nne.

Kwa ujio wake, Rashford hawezi kupata namba kikosi cha kwanza Man Utd lakini alifanya jambo kubwa sana katika mechi ya mwisho Ligi ya Uingereza alipofunga goli muhimu dakika za majeruhi dhidi ya Hull City.
Akizungumzia jukumu lake, Scholes anadai kuwa Rashford atapata nafasi nzuri ya kujifunza kutoka kwa Ibrahimovic msimu huu.

“Ibra ni mchezaji muhimu kwa wachezaji wadogo hasa kwa mtu kama Rashford,” alisema.

“Marcus atakuwa na majukumu makubwa katika msimu huu na kuwa mtu ambaye anaweza kujifunza kutoka kwake na kumfundisha namna ya kucheza vizuri. Ni jambo jema sana kwa mustakabali wake.”


Mourinho aliueleza ujio wa Ibra kama zawadi kwa maendeleo ya Rashford na Scholes anaoneka kuwa katika ukurasa mmoja na Mou.

No comments