MCHEZAJI tenisi mashuhuri Serena Williams ameondolewa kutoka kwenye mashindano ya wazi ya US Open jijini New York baada ya kushindwa hatua ya nusu fainali.
Ameshindwa na mchezaji wa Jamhuri ya Czech, Karolina Pliskova 6-2 7-6 (7-5).

Mchezaji huyo aliyeorodheshwa nambari moja duniani alikuwa anatumai kuweka rekodi kwa kushinda tuzo ya Grand Slam mara ya 23.

Lakini kwa sasa atasalia kushikilia rekodi na wachezaji wa zamani Steffi Graf katika mataji 22.
Matokeo hayo yana maana kwamba Serena Williams, 34, sasa atapitwa kwenye orodha ya wachezaji bora na Mjerumani Angelique Kerber.

Kerber amefikia fainali mara ya tatu 2016 na Mjerumani huyo alimshinda raia wa Denmark, Carolina Wozniack 6-4 6-3.

Serena mwenyewe amesema kwamba anajua kwamba mchezo huu una changamoto nyingi na si mara zote anazoweza kushinda.


“Wakati mwingine nashindwa na haya ndio matokeo ya mchezo wenyewe huu,” amesema. 
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac