SHAMSHA FORD AFICHUA HANA UHURU BAADA YA KUINGIA KWENYE MAISHA YA NDOA

MSANII wa filamu Shamsa Ford ameweka wazi kuwa maisha yake kwa sasa yamepungua uhuru baada ya kuingia katika ndoa tofauti na ilivyokuwa awali.

Nyota huyo alikiambia kipindi cha eNewz kuwa sio kama zamani alipokuwa akitoka “auti” mara kwa mara na badala yake hivi sasa anatumia muda mwingi kutulia nyumbani kwake.

“Mi bado ni M’ bongo Muvies na mume wangu ananielewa hivyo hakuna chochote kitakachobadilika ila ni kweli kwamba uhuru wa kutoka kama zamani umepungua," alisema Shamsa.


Shamsa aliongeza: “Ndoa yangu haijabadilisha miundo yangu wa uigizaji ingawa nalazimika kupunguza mambo mengine lakini kwenye filamu ninafanya kama kawaida.”

No comments