SHILOLE ASEMA HUWA ANAKUNYWA POMBE KUTOA NISHAI KABLA YA KUPANDA JUKWAANI

STAA wa Bongofleva Zuwena Mohamed “Shilole” Amesema anapofanya kazi ya muziki anahisi aibu hivyo hulazimika kunywa pombe kidogo ili achangamke kwanza.

Alisema kuwa kazi ya muziki ina changamoto zake zikiwamo za kufanya video za “Utata” ambazo wakati mwingine bila kunywa pombe kidogo msanii hawezi kuifanya kwa ubora unaotakiwa.

“Kwa mfano kwenye video "Natafuta Kiki" ya mdogo wangu Raymond ilibidi ninywe pombe kidogo ili nitoe aibu vinginevyo nisingeweza kushiriki kwa kupata ubora unaotakiwa,”alisema Shilole.


Alisema kuwa video hiyo ilikuwa kwake lakini akaona hana budi kumsaidia msanii huyo ndipo akavaa nguo za kulalia na kuingia mzigoni kwa kuingia kwenye sinki la kuogea alimoshutiwa.

No comments