SIKINDE YAPAGAWISHA BULYAGA TEMEKE KWA WIKI YA PILI JANA

MLIMANI Park Sikinde jana Ijumaa waliporomosha bonge la burudani ndani ya ukumbi wa Bulyaga Temeke na kukonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliohudhuria.
Vibao vyao vingi vikali kama vile “Teddy Mwana Zanzibar”, “Barua Toka kwa Mama” na “Deni Nitalipa” vilionekana kuusisimua zaidi umati wa watu waliohudhuria shoo hiyo.

Jana ni Ijumaa ya pili kwa Sikinde kutumbuiza ukumbini hapo na kukubalika baada ya wiki iliyopita ambapo kwa mujibu wa mratibu Juma Mbizo, watakuwa wakitumbuiza kila wiki.

No comments