MSANII wa muziki wa Bongofleva na filamu, Snura Mushi amefunguka na kusema kuwa yeye hana tabia ya kutoka kimapenzi na watoto wadogo kama kama baadhi ya wasanii wengine wa kike ama wanawake maarufu.

Snura aliyasema hayo kupitia kipindi cha eNEWS cha EATV na kudai alimkisi Raymond wakati anatengeneza video yake ya “Natafuta Kiki” kwa kudai kuwa pale alikuwa kazini ila sio kusema anatoka kimapenzi na msanii huyo kama ambavyo baadhi ya watu walivyoanza kuzusha.

“Baada tu ya kutoka ile picha, mimi na RayVanny  “tuki-kiss”, watu wakaanza kuniandika vibaya kwenye mitandao ya kijamii, sijui RayVanny ndie mwanaume aliyekuwa anamnyima usingizi Snura,” alisema Snura na kuongeza:


“Jamani RayVanny yule mimi ni mdogo wangu. Kazini naweza kumkisi hata mtoto wangu kama muvi ninayocheza inanambia nitembee na mwanangu. Katika maisha ya kawaida RayVanny ni mdogo wangu, mimi kusema ukweli huwa sina tabia ya kutoka kimapenzi na wadogo zangu.”
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac