STAMINA ASEMA YOUNG DEE AKIJIREKEBISHA WATAMREJESHA KUNDINI "WATU CHEE"... Young Dee mwenyewe adai hana mpango wa kurudi nyuma

MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya, Stamina amesema kuwa iwapo Young Dee atarekebisha makosa aliyofanya katika kundi la Watu Chee atarejeshwa katika kundi hilo kuendelea na kazi.

Young Dee aliondoka katika kundi hilo baada ya kupishana kauli kati yake na msanii mwenzake Country Boy ambaye walikuwa pamoja ndani ya kundi la Chee.

Hata hivyo Young Dee ametoa msimamo wake na kusema kuwa suala la yeye kwenda kuomba msamaa Watu Chee halipo kabisa na kwamba wanaomshauri aombe radhi wasipoteze muda wa kumuwazia.


“Mimi niwatakie kila la kheri katika safali hiyo ya kimuziki na nawaombea mafanikio huko mbeleni lakini suala la kurudi sidhani kama lipo tena,” alisema Young Dee.

No comments