TOTOO ZE BINGWA AREJEA MALAIKA BAND


UTAMU unazidi kukolea ndani ya Malaika Band chini ya Christian Bella baada ya mmoja wa wasanii waasisi wa bendi hiyo kurejea kundini.

Huyo si mwingine bali ni rapa mwenye vitu adimu Totoo ze Bingwa ambaye majuzi alikuwepo ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala na kupagawisha ile mbaya.

Totoo ameithibitishia Saluti5 kuwa amerejea Malaika na kuahidi kufanya makubwa chini ya boss Christian Bella.

“Nipo Malaika, namshukuru Bella kwa kunipa nafasi ya kuitumikia tena bendi hii, naahidi kumpa ushirikiano mkubwa,” alisema Totoo aliyepata kutamba sana na bendi za Beta Musica, FM Academia na Akudo Impact.

No comments