TOTTENHAM KUM-MISS MAJERUHI HARRY KANE KWA MIEZI MIWILI

TOTTENHAM wamo katika ofa ya presha kubwa ya kukosa huduma ya straika Harry Kane.

Kane ameumia kifundo cha mguu na sasa kuna taarifa kuwa anaweza kuwa nje ya dimba kwa miezi miwili.

Taarifa za ndani ya klabu ya Spur zinasema kuwa straika huyo analazimika kusubiri majibu ya vipimo vya kitabibu.

Awali Kane alihusishwa na tukio la kuvunjika kwa mfupa wake wa mguu, badala yake vipimo vya sasa vinasema ameumia kifundo alipoumia katika mechi iliyowakutanisha Spur na Sunderland katika mchezo wa Jumapili iliyopita.

Vipimo vilivyochukuliwa Jumatatu iliyopita vimetolewa ufafanuzi na kocha Mauricio Pochettino kwamba straika wake huyo ana tatizo kifundoni mwake.

“Kwa sasa Kane analalamikia maumivu makali na jambo lililo mbele yetu ni kuendelea kusubiri.”

Presha iliyo ndani ya Spur ni kutokana na kumtegemea straika mmoja tu aliyejiunga msimu huu ambaye ni Vincent Janssen.

Janssen alijiunga akitokea AZ Alkmaar, lakini hata hivyo hajabahatika kuifungia timu yake hiyo hata bao moja, hali inayomfanya kocha Mauricio kuwa katika presha kubwa juu ya kuumia kwa Kane.

No comments