UBELGIJI YAINYOA CYRPUS 3-0 NA KUMPA JEURI THIERRY HENRY… Lukaku moto chini

BAADA ya Ubelgiji kuinyoa Cyprus 3-0 kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2018, kocha msaidizi Thierry Henry amesema anaamini nchi hiyo ina kikosi imara kitakachoiteka dunia.

Ikitandaza soka la hali ya juu, Ubelgiji ikapata pointi tatu muhimu kwa mabao mawili ya Romelu Lukaku na moja la Yannick Carrasco.

Nyota huyo wa zamani wa timu ya Arsenal alichaguliwa hivi karibuni ili aweze kumsaidia kocha Roberto Marrntinez katika jukumu la kukinoa kikosi hicho.

Kwa uteuzi huo sasa Henry atakuwa akifanya kazi na wachezaji kama Eden Hazard Kevin de Bruyne na Romelu Lukaku ili kuhakikisha Ubelgji ikafanya vizuri baada ya kushindwa kuvuka hatua ya robo fainali katika michuano ya mataifa ya Ulaya "Euro 2016" ikiwa chini ya kocha wake wa zamani, Marc Wilmots.


“Ni changamoto kubwa mno lakini tunachokwenda kukifanya ni kuijenga timu kisaikolojia ili iweze kuwa tishio,” Henry aliiambia Sky Sports.

No comments