UNAMKUMBUKA FLORA MOSES WA EXTRA BONGO? KAWA CHA POMBE BALAA


ALIYEKUWA mwimbaji wa kike wa Extra Bongo ya awamu ya kwanza Flora Moses anadaiwa kuwa cha pombe (mlevi) kupindukia.

Miaka kadhaa iliyopita, Flora alikumbwa na tukio lililohusishwa na kubakwa kutokana ulevi wa kupindukia maeneo ya Kinondoni.

Lakini leo tena mwimbaji wa mwingine wa kike Tabu Mambosasa (pichani kushoto) ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa Flora anahitaji dua maana pombe zimemzidi na zinamzeesha.

Flora, pichani (kulia), aliunda safu ya hatari ya waimbaji wa Extra Bongo iliyoanzishwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Mwanadada huyo alikuwa sambamba na waimbaji kama Bashir Uhadi, Ally Chocky, Bob Kisa na Richard Maalifa bila kusahau Khalid Chokoraa na Grayson Semsekwa waliosimama pia kama marapa.
Hivi ndivyo alivyoandika mwimbaji Tabu Mambosasa (kushoto) kwenye ukurasa wake wa facebook kuhusu mwimbaji wa zamani wa iliyokuwa Extra Bongo Flora Moses (kulia)

No comments