VANESSA MDEE AZIMEZEA MATE TUZO ZA GRAMMY

MWANAMUZIKI Vanessa Mdee ana ndoto kubwa ambayo ni kutaka kuona siku moja anakuwa msanii kutoka Tanzania atakayeshiunda tuzo za heshima za "Grammy."

Vanessa anaamini kwamba mwanzo wa kukaribia ndoto zake umewadia na sasa ni mmoja ya wasanii wa Afrika waliochaguliwa kurekodi wimbo na mshindi wa Grammy na nyota wa R&B nchini Marekani, Rey Songz.

Akiwa pia anawania tuzo ya Loeries za Afrika Kusini kwa kazi yake ya video bora ya “Niroge”, Vanessa anaungana na Rema Namakula (Uganda), Yemi Alade (Nigeria), Neyma (Msumbiji), Serge Beynoud (Frech West Afrika), LIj Michael (Ethiopia), Stonebwoy (Ghana), Nyashimsiki (Kenya) na Emtee (Afrika Kusini) kurekodi wimbo wa Trey Songz.


“Katika harakati zangu kutafuta ushindi wa Grammy katika fani yangu ya muziki inanipa nguvu kufanyakazi kwa ukaribu na Trey Songz, ambaye alishawahi kushinda tuzo hiyo,” alisema Vanessa.

No comments