WAKALA WA BALOTELLI AAMINI MCHEZAJI WAKE ATAREJEA TENA ENGLAND

WAKALA wa mshambuliaji kutoka nchini Italia, Mario Balotelli, amesema anaamini iko siku mchezaji wake atarejea kucheza soka katika Ligi ya nchini England (EPL).

Mino Raiola ambaye ni wakala wa wachezaji wenye majina katika Ligi za barani Ulaya akiwemo Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic, ametanabaisha hayo kutokana na ubora wa kiwango cha Balotelli akiamini bado ana uwezo mkubwa wa kucheza katika klabu kubwa.

Kwa nyakati tofauti Balotelli ameshacheza kwenye Ligi ya nchini England katika klabu za Manchester City na Liverpool na amepitia changamoto kadhaa.

“Ufaransa inamwitaji kama ilivyokuwa ikimwitaji Zlatan. Yupo vizuri na iko siku atarejea katika Ligi ya nchini England,” alisema Raiola.

Balotelli alisajiliwa na klabu ya Nice baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp, jambo ambao lilipelekea kumweleza bayana kwamba hamwitaji katika kikosi chake.


“Mario ni Jurgen Klopp hawakupata nafasi ya kufanya kazi pamoja na Klopp hakutaka kumpa nafasi hiyo, Klopp alikuwa akimuona balotelli kama mpuuzi tu,” aliongeza Raiola.

No comments