WAKALA WA YAYA TOURE AMUONDOLEA UVIVU GUARDIOLA ...amwambia asijione mfalme kwa kushinda mechi chache, amtaka akafundishe Sunderland ili kudhihirisha ubora wake

Pep Guardiola has been blasted by Yaya Toure's agent over his handling of the midfielder

KOCHA wa Manchester City Pep Guardiola ameingia katika vita vya maneno na wakala wa Yaya Toure baada ya kukataa kumteua kiungo huyo katika orodha ya wachezaji 25 watakaoshiriki michuano klabu bigwa barani Ulaya katika hatua ya makundi.

Guardiola amesema hatamteua mchezaji huyo hadi pale wakala wake Dimitry Seluk, atakapoomba msamaha kwa matamshi aliyotamka kwa vyombo vya habari.

Lakini ajenti huyo amesema katu hatafanya hivyo na badala yake akasisitiza kwamba kocha huyo ndiye afaaye kuomba radhi.

''Kwa nini nimuombe msamaha Guardiola? Sijui maneno ninayostahili kutamka kuomba radhi, kwa sababu sijafanya kitu chochote. Iwapo nitajihisi kuomba radhi, basi nitaomba radhi hiyo, lakini sihisi kufanya hivyo. Kile Guardiola anachokitaka hakitawezekana,'' alisema Seluk kwenye maongezi yake na Sky Sport News.
Amesema kocha huyo amewakosea watu wengi akigusia mtangulizi wake Manuel Pellegrini na kisha kipa nambari moja wa Manchester City Joe Hart ambaye alilazimika kuondoka klabu hiyo majira ya joto baada ya kuachwa nje ya mipango ya Guardiola.
"Ni lazima awaombe radhi Yaya na Hart na Pellegrini. Guardiola anashinda mechi kadha na kuanza kufikiria kwamba yeye ni mfalme."
"Guardiola sio kocha wa ajabu, mafanikio ya Barcelona yaliletwa na Lionel Messi, sio yeye. Hata babu yangu angeweza kutwaa ubingwa kama angekuwa kocha Bayern Munich.
"Anabebwa na ukubwa wa timu na umahiri wa wachezaji, kama Guadiola  anajiamini kuwa yeye ni kocha bora basi akafundishe Sunderland," alisema Wakala huyo wa Toure.
Seluk amesema mteja wake, Toure, 33, ameshiriki katika mechi moja kati ya mechi nane walizozicheza Manchester City msimu huu.
Guardiola amesema iwapo Seluk atamuomba msamaha yeye, klabu hiyo na wachezaji wa timu hiyo hapo ndio Yaya atakuwa na nafasi sawa ya kushiriki katika michezo yote.
''Sitakubali kama kocha kila ajenti, kwenda kwa vyombo vya habari kuwasilisha malalamiko yao iwapo mchezaji wake hajashirikishwa kweye kikosi," Guardiola ameongezea.
Guardiola alikuwa kocha mkuu Barcelona wakati Toure alipouzwa kwa Manchester City mwaka 2010.


No comments