WATU WANAFIKI WAMCHEFUA WEMA SEPETU... akana kuhusika kuanzisha "Team Wema"

WEMA Sepetu amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake huwa hapendi watu wanafiki kwa madai kuwa watu wa aina hiyo ni hatari kwa maendeleo yake.

Wema alisema hayo alipokuwa akizungumzia changamoto alizozipitia ambazo amekuwa akikutana nazo tangu awe maarufu na kudai kwamba sasa amechoka kuzushiwa mambo ya kinafiki.

Alisema kuwa watu wamekuwa wakiunda makundi yao kwenye mitandao ya kijamii na kisha wanayapa majina ya "Team Wema" bila yeye kujua na kumsababishia usumbufu.

Kimwana huyo anajua kuna watu wanampenda  na anashukuru kwa sapoti yao, lakini si kwamba yeye ndiye aliyeunda Team Wema, hivyo anawashangaa wanaompigia simu na kumuomba awaunganishe kwenye "Team Wema."

No comments