WENGER AAMINI JACK WILSHERE “NI WA ARSENAL TU”

KOCHA Arsene Wenger amesema matumaini yake ni kwamba kiungo wa kati, Jack Wilshere ambaye kwa sasa ametumwa Bournemouth kwa mkopo atasalia Arsenal maisha yake ya uchezaji.

Wilshere mwenye umri wa miaka 24, ambaye huichezea timu ya taifa ya Uingereza, alienda Bournemouth kwa mkopo wa msimu mmoja.

Ni mmoja wa wachezaji waliokua kutoka chuo cha kustawisha wachezaji cha Arsenal na aliwachezea mechi yake ya kwanza 2008 akiwa na miaka 16.

Lakini alicheza mechi tatu pekee katika klabu hiyo msimu uliopita kutokana na majeraha.

“Yeye ni mchezaji stadi sana, hahitajiki kufanya jambo lingine kunionyesha uwezo wake,” amesema Wenger.
“Binafsi natumai atasalia hapa maisha yake yote ya uchezaji.”


Wenger amesema walizungumza na mchezaji huyo na amekuwa akiamini kwamba kuna siku atakuwa mchezaji tegemeo wa Arsenal kuliko ilivyo wakati huu.

No comments