Habari

WENGER ASEMA CHELSEA BILA TERRY NI UCHOCHORO

on

JUMAMOSI hii litapigwa pambano
la kukata na shoka la ligi kuu ya englkand jijini London kati ya matajiri wa
jiji la Chelsea watakaokuwa wageni wa Arsenal kwenye dimba la Emirates.
Umemsikia kocha wa Arsenal, Arsene
Wenger? Amesema siku hiyo hatokubali kuachia pointi tatu ziende kwa matajiri
hao wakati anaijua timu hiyo kwa sasa ni ya kuungaunga.
Wenger amesema Chelsea bila
nahodha wao John Terry ni kichochoro cha kuvunia pointi kwa kila timu, hivyo
atahakikisha vijana wake wanabakiza pointi zote tatu.
“Najua Chelsea watataka
kushinda Jumamosi, lakini naamini tutawashinda kwa sababu wanapomkosa Terry
wanacheza ovyo kwenye ulinzi na tutalitumia pengo hilo kikamilifu,” alitamba
Wenger.

Chelsea wataingia dimbani
wakikumbukia maumivu waliyoyapata Ijumaa iliyopita walipopigwa mabao 2-1 na
Liverpool kwenye dimba lao la Stanford Bridge kikiwa ni kipigo cha kwanza kwa
msimu huu katika Ligi Kuu.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *