WENGER HAFAHAMU NI KWANINI ALIMRUHUSU SANCHEZ KUPIGA PENATI

KOCHA Arsene Wenger amekiri akisema kwamba hafahamu ni kwa nini aliamua Alexis Sanchez apige penati iliyookolewa badala ya Santi Cazorla katika mchezo wa Ligi Kuu ambao waliondoka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Hull City.

Katika mchezo huo wa juzi Sanchez alishaingia katika orodha ya wafungaji wa Arsenal na kisha akafunga mabao matatu lakini jitihada zake za kutaka zaidi zikatibuliwa na mlinda mlango wa Hull City, Eldin Jakupovic baada ya kuokoa mkwaju wake wa penati katika klabu hiyo.


“Santi ndio aliyepaswa kupiga penati hiyo. Siwezi kufahamu ni kwa nini haikuwa hivyo, sikupanga Sanchez apige penati hiyo,” alisema Wenger katika mahojiano yake na shirika la utangazaji la Uingereza (BBC).

"Nahitaji kufahamu kilichotokea na sitaki kitokee tena. Kwa ujumla tunafahamu kila mtu anaweza kukosa penati, tunakubaliana na jambo hilo na hii inaweza kumtokea Santi Cazorla," aliongeza Mfaransa huyo.

No comments