WIMBO "MATATIZO" WA HARMONIZE WAMKUNA JAKAYA KIKWETE

WIMBO matatizo wa msanii wa Bongofleva, Harmonize ni moja kati ya nyimbo ambazo zimependwa na rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

Wiki iliyopita Mh rais mstaafu, Jakaya Kikwete aliwaalika viongozi wa WCB pamoja na wasanii wake nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana.

“Unajua wakati Mh Jakaya Kikwete anatoka madarakani Diamond Platnumz bado alikuwa hajasaini wasanii wengine chini ya WCB, hivyo tulikwenda kuwatambulisha kina Harmonize, Raymond  pamoja na Rich Mavoko pia kukabidhi kazi zao, lakini uzuri wakati tunakabidhi kazi Mh Kikwete alikuwa amevutiwa na wimbo wa Harmonize wa matatizo akawa anasema alikuwa kwenye gari akiusikiliza na kusema kuwa kijana ameimba sana,” Sallam alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.


Sallam alisema hatua ya kukutana na JK wana imani itawasaidia kuwapa Connection katika muziki wao.

No comments