Habari

YAYA TOURE AHOFIA MAAMUZI YA FIFA YATACHOCHEA UBAGUZI WA RANGI

on

Yaya Toure has hit out at FIFA's decision to disband their anti-racism task force
KIUNGO wa Manchester City, Yaya
Toure amesema wachezaji na mashabiki wanaweza kuumia kufuatia hatua ya
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuvunja kikosi kazi kilichoundwa kwa ajili ya
kupambana na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika soka.
Toure mwenye umri wa miaka 33, alikuwa mmoja wa wajumbe
katika kikosi kazi hicho kilichoundwa mwaka 2013 kusaidia kutokomeza ubaguzi.
Katibu mkuu wa FIFA, Fatma Samba Diouf Samoura amesema
kikosi kazi hicho kilikuwa na kazi maalumu ambayo tayari wameimaliza.
Hata hivyo, hatua hiyo imekosolewa vikali na wadau
mbalimbali, akiwemo Toure ambaye alifanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki
wa CSKA Moscow Octoba mwaka 2013.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast amesema
hatua hiyo ya FIFA itaweza kuwaumiza mashabiki na wachezaji kama mipango sahihi
isipowekwa.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *