YAYA TOURE BADO “ANA IMANI” NA MANCHESTER CITY

PAMOJA na kwamba hana uelewano mzuri na na kocha wake, kiungo nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure amesema bado hajakata tamaa ya kuitumikia klabu ya Manchester City licha ya kuenguliwa kwenye kikosi kitakachoshiriki Ligi ya Mabingwa msimu wa 2016/17.

Toure ameonyesha ujasiri wa kutaka kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Etihad  Stadium wakati alipohojiwa na gazeti la Daily Mail la nchini England na kusema anajipanga kuwasilisha maombi ya kutaka asaini mkataba mpya.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, amekuwa katika hali ya sintofahamu dhidi ya meneja mpya wa Manchester City, Pep Guardiola, jambo ambalo limezua hofu ya wawili hao kutopika chungu kimoja tangu wakiwa FC Barcelona.


Mwanzoni mwa juma hili, wakala wa Toure (Dimitri Seluk), alisema huenda mchezai wake akasaka mbinu za kuihama Man City wakati wa majira ya baridi mwezi Januari kufuatia mazingira yaliyomzunguuka huko Etihad Stadium tangu alipowasili Pep Guardiola.

No comments