YAYA TOURE KUIMWAGA MANCHESTER CITY JANUARI

WAKALA wa mchezaji mahiri na nahodha wa Ivory Coast, Yaya Toure, amesema kuwa mchezaji huyo atavunja mkataba wa kuitumikia timu hiyo Januari mwakani.

Dimitri seluk amefichua kuwa Toure hajafurahishwa na kitendo cha kuachwa nje ya kikosi cha City kitakachoshiriki michuano ya Ligi ya Maibingwa Ulaya.


Bila shaka sasa imethibitika kuwa Guardiola ambaye alimuuza Tore wakati alipotwaa ukocha kwenye timu ya Barcelona, angali na chuki binafsi na mchezaji huyo, mmoja wa viongo bora duniani kwa sasa.

No comments