YUSUPH MDOE NA WENZAKE WAENDA AZERBAIJAN KUIWAKILISHA TZ KATIKA CHESS OLYMPIAD 2016


TIMU ya Taifa ya  Tanzania kwa mchezo wa Chess  imeondoka nchini Jumatano jioni kwenda Azerbaijan kwenye michuano ya Chess Olympiad 2016.

Timu hiyo ambayo inawakilishwa na wachezaji sita kwa timu ya wanaume na sita kwa wanawake, itakuwa miongoni mwa nchi takriban 180 zitakazoshiriki michuano hiyo.

Michuano hiyo yenye hadhi kubwa kama ya Olimpiki, inafanyika katika mji wa Buku kuanzia Septemba Mosi hadi Septemba 14.

Wachezaji hao kwa upande wa wanaume ni Geoffrey Mwanyika, Mbwana Khojana, Nurdin Hassuji, Hemed Mlawa, Yusuph Mdoe na Mwaisumbe Emanuel.

Timu ya wanawake inaundwa na Kangwa William, Fena Ngwamwambwa, Aida Lalika, Martha Anawa, Vidah Femmie na Navin Choudary.
Pichani juu ni baadhi ya wachezaji wa Tanzania Mbwana Khojana (kushoto) na Yusuph Mdoe wakiwa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatano jioni tayari kwa safari ya Azerbaijan.

No comments