ZIDANE ASEMA HANA WASIWASI NA RONALDO, ANAMWAMINIA

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa hana wasiwasi kuhusu kiwango cha straika wake, Cristiano Ronaldo, baada ya Mreno huyo kushindwa kuziona nyavu katika mchezo wa usiku wa kuamkia juzi ambao walikwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya Villarreal.

Ronaldo alikosa mechi ya Kombe la UEFA Super Cup dhidi ya Sevilla na mechi mbili za La Liga kutokana na majeraha ya goti ambayo aliyapata wakati wa fainali za mataifa ya Ulaya “Euro 2016”.

Lakini aliweza kurejea uwanjani kati amchezo walioibuka na ushindi wa mabao 5-2dhidi ya Osasuna kabla ya kuiongoza Real Madrid kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sporting CP katika Ligi ya Mabingwa ambapo aliweza kufunga bao kila mechi.

Hata hivyo usiku wa kuamkia juzi staa huyo mwenye umri wa miaka 31 hakuweza kuziona nyavu dhidi ya Villareal ambapo Real Mdrid walipoteza pointi kwa mara ya kwanza na Zidane anaona hana haja ya kuumia kichwa.

“Kutokana na ninavyomuheshimu Cristiano, sina wasiwasi naye na pia ni mchezaji muhimu kwetu sisi dhidi ya Villareal kama alivyo mara zote,” Zidane aliwaambia waandishi wa habari.


“Sina hofu asipofunga. Jambo la muhimu ni kwamba yupo uwanjani anatupigania. Huwa ninakuwa na hofu anapokuwa nje ya uwanja,” aliongeza kocha huyo.

No comments