Habari

ZINEDINE ZIDANE AKUBALIKA REAL MADRID… mashabiki wapanga kumuaga kwa heshima atakapoondoka

on

WAKATI kiungo fundi wa zamani,
Zinedine Zidane raia wa Ufaransa akikabidhiwa mikoba ya ukocha wa mabingwa wa
Ulaya, Real Madrid Januari mwaka huu, ni wadau wachache wa soka waliomkubali.
Wapo waliosema bora Madrid
wangebaki na kocha wao Rafa Benitez kuliko kumpa Zidane kibarua hicho ambacho
hana uzoefu nacho.
Kipigo cha mabao manne kwa bila
kutoka kwa wapinzani wao wakuu, Barcelona kiliongeza joto kwa mashabiki lakini
viongozi wa Madrid hawakutetereka, walimwamini Zidane na miezi mitano baadae
akawapa ubingwa wa Ulaya kabla ya kuwaongezea taji la ubingwa wa Super League.
Hivi sasa mashabiki wa Real
huaambii chochote kwa Zidane, wanaamini chini yake watarudisha enzi za mataji
Santiago Bernabeu na wameshasema hata ikibidi kuondoka kwenye nafasi hiyo,
watamuaga kwa heshima.
Zidane amefikia rekodi ya Pep
Guardiola aliyeiongoza Barca kushinda mechi 16 mfululizo mechi za Ligi Kuu
msimu wa mwaka 2010/11.
Real wanaongoza Ligi Kuu
Hispania hadi sasa, walishinda mechi 12 mfululizo za mwishoni mwa msimu
uliopita na msimu huu weshashinda mechi zote nne za kwanza.

Chini ya Zidane Madrid imecheza
mechi 33, imepoteza mbili, imetoka sare tano na kushinda mechi 26 za michuano
mbalimbali.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *