ZLATAN IBRAHIMOVIC AFANANISHWA NA ROBOT

Manchester United striker Zlatan Ibrahimovic issues instructions to team-mates 
ZLATAN IBRAHIMOVIC amekuwa akiitwa majina mengi sana katika historia yake ya soka, lakini sasa amefananishwa na roboti au Terminator.

Sentahafu wa Northampton, Gabriel Zakuani amesema mshambuliaji huyo wa Manchester United anaongea kama robot au Terminator.

Zakuani ameiaimbia BBC: "Anaongea sana uwanjani, lakini anaongea kwa sauti kama ya robot au Terminator, ni kama sauti ambayo iko kwenye 'slow motion'.

"Unaweza ukaona namna anavyowahamasisha wachezaji wanzake. Ataawaambia wachezaji wachache wanaokimbia mbele yake kutulia na na kuondoa shaka wanapokuwa na mpira.

"Ni mtu anayejituma bila kuchoka na anaonyesha kumuheshimu kila mmoja katika timu yake."

The 34-year-old striker is challenged by Zander Diamond (right) and Gabriel Zakuani (left) 
Ibrahimovic akichuana na Zander Diamond (kulia) na Gabriel Zakuani (kushoto) 
The Terminator is a science fiction franchise which includes five films to date
Terminator sayansi ya kufikirika iliyohusika katika sinema tano zilizopata umaarufu mkubwa duniani
The Sweden legend limbers up on the touchline before playing at the Sixfields Stadium
Ibrahimovic akipasha mwili moto kabla ya kuingia uwanjani

No comments