ZLATAN IBRAHIMOVIC ASEMA ANAJIVUNIA KUFANYA KAZI TENA NA MOURINHO

STRAIKA Zlatan Ibrahimovic amesema kwamba hana kitu kingine ambacho anaweza kujivunia katika kibarua chake kama kufanikiwa kufanya kazi na kocha wake, Jose Mourinho baada ya wawili hao kuungana tena Manchester United ikiwa ni baada ya kufanya kazi pamoja katika timu ya Inter Milan.

Straika huyo na kocha wake walifanya kazi pamoja kwa mwaka mmoja kwenye klabu hiyo ya Sansiro kabla ya Ibrahimovic kwenda kujiunga na Barcelona na huku Mourinho akilazimika kupata ubingwa wake baada ya mwaka mmoja.

Akizungumza kabla ya mechi ya juzi dhidi ya Manchester City ambapo Ibrahimovic alikuwa akimkabili kocha wake wa zamani wa Barca, Pep Guardiola, staa huyo mwenye umri wa miaka 34 alimmwagia sifa kocha wake huyo wa Man United.

“Mourinho ni mtaalam kwani anafahamu kila kitu kuhusu mechi,” alisema straika huyo.


“Sina kitu kingine cha kujutia bali ni kutocheza muda mrefu chini ya Mourinho na nafasi iliyokuja ili awe kocha wangu Man United ulikuwa ni uamuzi rahisi,” aliongeza staa huyo.

No comments