ALEXANDER HLEB AAMINI ARSENAL YA MWAKA HUU ITAZOA MATAJI MATATU

KIUNGO wa Arsenal Alexander Hleb anaamini kuwa kikosi cha sasa cha kocha Arsene Wenger kina uwezo wa kushinda mataji matatu msimu huu.

Gunners wamekuwa na mwanzo mzuri msimu huu wakiwa nyuma kwa pointi mbili kutoka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England.

 Hleb aliyecheza bila mafanikio akiwa Arsenal baada ya kushindwa kutwaa mataji hata moja anaamini kikosi cha sasa cha Wenger kinaweza kutwaa mataji mkadhaa.

“Natumai timu itawaa mataji matatu msimu huu. Ligi Kuu Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya,” alisema Hleb wakati akizungumza na Reuters.


"Arsenal inaonyesha ina uwezo wa kufanya vizuri nitakuwa nyuma yake kuisaidia."

No comments