MENEJA wa msanii wa Bongofleva nchini, Ali Kiba, Aidan Charlie  ameibuka na kudai kuwa sababu iliyosababisha msanii huyo kushindwa ku-perform kwenye tamasha la Mombasa Rocks Festival ni kutokana na muda kushindwa kuwa rafiki.

Meneja huyo alieleza kuwa shoo hiyo ilitakiwa ianze mchana lakini ilianza muda ambao ilisababisha shoo hiyo kushindwa kumalizika kwa wakati.

“Ishu kubwa iliyokuwepo ni muda, shoo ilitakiwa kuanza saa nane mchana na kumalizika usiku kama saa sita, lakini kutokana na wenyewe waandaji walivyojipanga mambo hayakwenda kama walivyokusudia, kwahiyo badala ya kuanza shoo saa nane ikaanza saa tatu usiku.”


“Lakini shoo ilipoanza walitumbuiza Navio, Vanessa hata Naziz akaondolewa,” alisema meneja Aidan.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac