AMBER LULU AMUUMBUA YOUNG DEE KUHUSU UHUSIANO WAO

BAADA ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini rapa Young Dee kukanusha madai ya kutoka kimapenzi na mwanadada mrembo Video queen Amber Lulu, mwanadada huyo ameibuka na kuthibitisha kuwa madai hayo yana ukweli.

Amber Lulu amefunguka ukweli kwa kusema kwamba amekuwa na uhusiano na rapa huyo kwa tangu miaka minne iliyopita wakati akiwa mkoani Mbeya.


“Marafiki zangu wanajua ni jinsi gani nilivyokuwa naishi naye, mara ya mwisho alikamatwa na polisi mimi ndio nilienda kumtoa ndugu zake wote walikataa kwenda mimi nimeenda. Inamaana matatizo yangu yeye anayafurahia?"

"Sikuwa nimefanya vile kwa kuwa alikuwa ni mpenzi wangu ni mtu ninayemfahamu siku nyingi na ambaye tupo wote,” amesema Amber.

No comments