ANDER HERRERA AITWA MARA YA KWANZA KIKOSI CHA HISPANIA

KIUNGO wa Manchester United, Ander Herrera amefanikiwa kuitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Hispania kitakachocheza mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

Awali kiungo huyo alikuwa ameshachezea timu za vijana wenye umri chini ya miaka 21 na 23 lakini alikuwa hajawahi kuitwa kwenye kikosi cha timu ya wakubwa.

Hata hivyo, bada ya Herrera kuonyesha kiwango kizuri katika michuano ya Ligi Kuu England, kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Julen Lopetegui ameridhika na kumwita kiungo huyo katika kikosi chake kitakachoivaa Italia na Albania.

Baada ya kukaa benchi kwa muda wa wiki chache lakini Herrera kwa sasa amelazimisha kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho na anaonekana kushirikiana vizuri na kiungo mshambuliaji, Paul Pogba.

No comments