ANDY COLE AIPA "TANO" LIVERPOOL AKISIFIA SOKA LAO

MANCHESTER United kesho itakuwa mgeni wa Liverpool katika dakika 90 kali za Ligi Kuu England kwenye uwanja wa Anfield.

Lakini kabla hata ya mchezo huo, mkongwe wa mashetani wekundu, Andy Cole ameipa ‘dole’ Liverpool ya kocha Mjerumani Jurgen Klopp akisema aina ya soka wanalocheza ni sawa na utamu ambao huwezi kuuelezea.

Hakuishia hapo tu, akasema zaidi kuwa msimu huu Liverpool washindwe wenyewe kubeba ndoo ya Ligi Kuu.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa United, 45, anaamini Klopp amefanikiwa kuibadilisha Liverpool hadi kucheza soka la kuvutia kuangalia na la ushindani pia.

“Unajua Liverpool ninaipendea nini? Napenda jinsi washambuliaji wanavyocheza,” alisema Cole.

“Nadhani washambuliaji wanacheza soka tamu, mabao yanakuja kutoka kila upande.

“Klopp amemleta sadio Mane, nimemtaja mara kadhaa Daniel Sturrdge, mmoja wa washambuliaji wa kati bora kabisa England.”


“Unapokuwa na wachezaji kama hawa lazima ufunge mabao na pia utengeneze nafasi za kufunga.”

No comments