ANTHONY JOSHUA AAFIKI KUZICHAPA NA VLADIMIR KLITSCHKO

BONDIA Mwingereza Anthony Joshua ameafiki vipengele vya mkataba kwa ajili ya pambano lake la kuwania mkanda wa uzito wa juu duniani dhidi ya Vladimir Klitschko.

Lakini promota Eddie Hearn anataka kwanza kuthibitisha ni mikanda mingapi itapiganiwa siku hiyo kabla ya kutangaza pambano hilo litakalofanyika Desemba 10 au 17, kwenye ukumbi wa Manchester Arena.

Joshua atatetea taji lake la IBF, wakati IBO wamekubali mkanda wao upiganiwe na promota Hearn anaafikiana na WBA na WBO kujaribu kuwashawishi waijumuishe mikanda yao katika pambano hilo.

“Kimsingi dili limekamilika kwa upande wetu na Klischko,” alisema promota Hearn. “naweza kusema vipengele vya mkataba vimeafikiwa, lakini kuna mambo yanayosubiriwa ili mkataba usainiwe.”

“Tunahakikisha pale tutakapotangaza tutangaze mikanda gani itagombewa kuliko kutangaza mikanda miwili kasha mingine iongezwe baadae.”


No comments