ARSENAL "KIDUME" KUIVAA LUDOGORETS NYUMBANI KWAO EMIRATES LEO

HAKUNA ubishi kwamba Arsenal kwa sasa wako vizuri, wameshinda mechi sita za mwisho mashindano yote na leo watakuwa wenyeji wa Ludegorets kwenye dimba la Emirates katika mechi ya Ligi ya mabingwa Ulaya.

The Gunners waliichapa Basel katika mechi yao iliyotangulia na sasa wanaongoza Kundi wakiwa na pointi nne baada ya mechi mbili.

Lakini pia kikosi cha kocha Arsene Wenger kinashuka dimbani kikijivunia rekodi ya kucheza mechi 10 bila kupoteza mashindano yote, kikishinda mechi nane na sare mbili.

Wapinzani wao, Ludogorets walikumbana na kipigo cha mabao 3-1 katika mechi yao ya mwisho kutoka PSG.

Pamoja na kuwa hawajafanya vizuri katika michuano hiyo Ulaya, lakini kwenye Ligi ya nyumbani Ludogorets wako vizuri wakishika nafasi ya pili kwenye msimamo.

Katika mtanange mwingine, wageni kwenye michuano hiyo, Rostov ya Russia baada ya sare ya 2-2 dhidi ya PSV Eindhoven, watakuwa nyumbani wakiisubiri Atletico Madrid iliyoshinda bao 1-0 katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Bayern Munich.


Kwa upande wao, mabingwa wa Ujerumani watakuwa wenyeji wa PSV Eindhoven katika mechi nyingine ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ujerumani.

No comments