ARSENE WENGER AELEZEA UMUHIMU WA "WATU WAZIMA" KWENYE KIKOSI

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameelezea umuhimu wa kuwa na wachezaji wenye uzoefu na akasema kuwa ili timu iweze kuota mafanikio ni lazima iwe na wachezaji wenye umri wa kati ya miaka 23 na 30.

Kwa muda mrefu Wenger amekuwa akishutumiwa kwa kutumia wachezaji makinda lakini akawa anafumba macho lakini sasa inavyoonekana amebaini kuwa timu yenye wachezaji chipukizi haiwezi kutwaa ubingwa wowote mkubwa.

“Ili uweze kuwa mchezaji wa kweli ni lazima uwe na miaka walau 23 kwasababu utakuwa umeshajifunza kazi, unaweza kucheza mechi kubwa wakati mwingine za kulipiza kisasi,” ya miaka 23 na 30.

Kwa muda mrefu Wenger amekuwa akishutumiwa kwa kutumia wachezaji makinda lakini akawa anafumba macho lakini sasa inavyoonekana amebaini kuwa timu yenye wachezaji chipukizi haiwezi kutwaa ubingwa wowote mkubwa.

“Ili uweze kuwa mchezaji wa kweli ni lazima uwe na miaka walau 23 kwasababu utakuwa umeshajifunza kazi, unaweza kucheza mechi kubwa wakati mwingine za kulipiza kisasi,” Wenger aliiambia tovuti ya klabu hiyo.

“Unaweza kuwa na vipaji vya ziada viwili ama vitatu, lakini kwa sasa tuna wachezaji kama Hector Bellerin na Alex Iwobi, lakini idadi kubwa ya wachezaji wana umri kuanzia miaka 23 na 30,” aliongeza Mfaransa huyo.


Alisema hata ukiangalia kwa upande wa timu za taifa, unapokuwa na timu ya wachezaji chipukizi huwezi kutwaa ubingwa kwa sababu wanakuwa hawana mawazo ya kutwaa ubingwa.

No comments