ARSENE WENGER AOMBA RADHI MASHABIKI WA ARSENAL AKIJIANDAA KUONDOKA

UPO uwezekano mkubwa kocha king'a’g'anizi uwanja wa Emirates, Arsene Wenger asiwe tena kocha wa Arsenal msimu ujao baada ya miaka 20 ya kufundisha.

Wakati mwenyewe pia akifahamu kuwa huenda akaondoka Gunners, amesifu uvumilivu walioonyesha mashabiki wa klabu hiyo dhidi yake na amewaomba radhi.

Kocha huyo raia wa Ufaransa ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu alisema hayo juzi.

Wakati wote aliokuwa madarakani Wenger ameongoza timu hiyo kutwaa mataji makubwa tisa yakiwemo ya Ligi Kuu na Kmbe la FA.

 “Ni kweli miaka 20, naomba samahani,” alisema Wenger “Ningependa kuwashukuru kwa msaada wenu kwa kipindi chote hicho. Nawaomba samahani kwa kila dakika iliyokutana na mambo ambayo hakimpenda kutoka kwangu kwa miaka 20.

“Nawaomba samahani kwa kijana aliyezaliwa miaka 20 na kushuhudia kocha mmoja tu Arsenal, napenda kumfahamisha kijana huyo kuwa atakapofikisha miaka 40 kuna mambo kadhaa atakuwa amejifunza."

“Nimejaribu kufanya mazuri kwa miaka 20 kwa klabu hii. Nilijitoa kwa hali na mali kuitumikia klabu, kwa kipindi chote nimekuwa nikithamini kazi yangu na kufanya kwa mapenzi makubwa. Nilimheshimu kila mmoja na msingi wa kuleta maendeleo kwenye klabu.”

Wakati huohuo, mwenyekiti wa Arsenal, Chips Keswick amesema suala la mkataba wa Wenger mara muda wake utakapomalizika sio jambo muhimu la kuzungumza wakati huu.

No comments