ARSENE WENGER SASA AKOMAA KWA AUBAMEYANG...

KOCHA Arsene Wenger ameamua kuacha uvivu wa usajili ambapo sasa ameingia katika vita ya kumwania nyota wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang.

Habari zilizopatikana juzi kutoka mitandao ya kimataifa zinasema kwamba Arsenal imepania kumalizana na mchezaji huyo raia wa Gabon katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo mwezi Januari kwa kitita cha pauni mil 52.

Arsenal ilitumia kiasi cha pauni mil 17 msimu huu kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Deportivo la Coruna, Lucaz Perez kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili msimu huu.

Kocha wa washika bunduki hao, Arsene Wenger alihamishia akili yake kwa Perez baada ya kushindwa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Leicester City, Jamie Vardy lakini pia nyota wa Lyon ya Ufaransa Alexandre Lacazette.

Sasa akili ya Wenger ni kwa nyota huyo wa kimataifa wa Gabon ambaye amekuwa katika kiwango cha juu sana kwenye timu yake ya sasa nchini Ujerumani.

“Pierre-Emerick Aubanyange yuko kwenye kiwango cha juu kabisa na haitakuwa ajabu kumsajili. Unaweza kufanikisha uwezo wake wakati ule tulipomsajili Nwanko Kanu wa Nigeria au Emmanuel Adebayor wa Togo,” amesema Wenger.

Lakini mtandao mwingine wa El Confidencial umedai kwamba inawezekana kabisa Aubameyang akahamia Arsenal mwezi Januari lakini si kwa kiwango ambacho kinatajwa.


Dortimund wanadaiwa kwamba wamekataa ofa hiyo na wanataka walipwe Euro mil 100 sawa na pauni mil 86. 7 kama kweli Arsenal wanaitaka huduma ya nyota huyo.

No comments