AUBAMEYANG ASHINDWA KUCHAGUA TIMU YA KUJIUNGA NAYO NA KUBAKI NJIAPANDA

MSHAMBULIAJI mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao, Pierre-Emerick Aubameyang amesema yuko njia panda asijue aichague timu gani ya kujiunga nayo.

Nahodha huyo wa Garbon anayeitumikia Borussia Dortmund ya Ligi Kuu Ujerumani amesema timu hizo zote zimefanya mazungumzo na wakala au baba yake mzazi.

“Kwa kweli nipo katika wakati mgumu wa kuchagua pa kwenda, Manchester City wameamua na baba yangu kunitaka nijiunge nao, wakati Real Madrid na Paris Saint-Germain wamezungumza na wakla wangu,” alisema Aubameyang.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 ambaye amekuwa nguzo ya mabao ya Borussia Dortmund kwa misimu mitano mfululizo, alisema anapitia kipindi kigumu hivi sasa.


City chini ya Pep Guardiola wamemtengea pauni mil 65 za uhamisho kutokana na kukunwa na uwezo wake ambapo hadi sasa ameshafunga mabao saba na kutengeneza mengine kadhaa.

No comments